Alhamisi 26 Februari 2026 - 16:20
Uhispania yataka Umoja wa Ulaya kutumia nyenzo za shinikizo dhidi ya utawala wa Kizayuni

Hawza/ José Manuel Albares, Waziri wa Mambo ya Nje wa Spain, katika hotuba yake kuhusu kuendelea mgogoro wa kibinadamu huko Ghaza na kuendelea kwa ujenzi wa makazi ya walowezi wa utawala wa Israel katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu, alitaka msimamo madhubuti zaidi kutoka Ulaya.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Albares alisema kuwa; mauaji ya watu bado yanaendelea huko Ghaza mikononi mwa utawala wa Kizayuni, huku misaada ya kibinadamu ikiwa imehifadhiwa katika vivuko vya mipakani na utawala huo na haingii Ghaza.

Aliongeza kuwa; ukimya wa Umoja wa Ulaya kuhusu uvamizi wa Israel katika Ukingo wa Magharibi na juhudi za kuwahamisha na kuwafanya Wapalestina kuwa wakimbizi haueleweki, na akataka kuchukuliwa kwa msimamo ulio wazi zaidi na unaoendana na misingi ya kibinadamu na kimaadili iliyotangazwa na umoja huo.

Albares alisema kuwa: Umoja wa Ulaya una nyenzo zinazohitajika za kuuwekea shinikizo utawala wa Israel, na aliutaka umoja huo kuzitumia ili kukabiliana na kuzorota kwa hali ya kibinadamu na kuendelea kwa ujenzi wa makazi ya walowezi.

Aidha, katika taarifa tofauti, alikosoa ushuru wa Marekani na kuuelezea kuwa ni shambulio dhidi ya mamlaka ya Ulaya.

Chanzo: Middle East Monitor

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha